Umewahi kusikia mtu anakuambia ili ufanikiwe kiurahisi ni Lazima Ujiposition..
Mwingine utasikia anasema, ili ifanikiwe ni lazima uchague NICHE..
Ofcourse wana Hoja za Msingi wasikilize, nadhani kitu cha msingi ambacho huwa hawakuambi ni kwamba wanaposema Jiposition huwa wana Maana gani na wanaposema chagua NICHE huwa wana maana gani..
Iko hivi...
NICHE ni kundi dogo ambalo Mfanyabiashara au mtoa huduma amelichagua kama SOKO LAKE, kwahiyo yeye anatatua changamoto au anasaidia mahitaji ya watu wa kundi hilo.
Mfano:
MFANYABIASHARA anaweza kusema yeye atakua anauza bidhaa za ELECTRONIC peke yake, maana yake amechagua WATEJA wa bidhaa za Electronic ndio atakua anawahudumia.
MTOA HUDUMA anaweza kusema mimi nitasaidia WANAOTAKA KUFANIKIWA kwenye mtandao wa INSTAGRAM, maana yake huyu kachagua niche ambayo ni mtandao wa INSTAGRAM
POSITIONING kwa lugha rahisi ni kuchagua aina ya bidhaa au huduma utakayokua unahusika nayo kutoka katika NICHE/SOKO uliyochagua..
Mfano:
Yule Mfanyabiashara wa Electronic yeye akaamua kusema katika bidhaa zote za Electronic mimi nitauza TV PEKEE kwa kiasi kikubwa, nataka watu wakitaka TV za uhakika wanicheki mimi, so ameamua kujipostion kama mtaalamu au mtu noma kabisa kwenye kuuza TV, "Specialization"
Yule mtoa huduma wa kusaidia Wafanyabiashara wanaotaka kukua katika Instagram yeye akaamua kusema kwamba mimi nitajiposition kama mtaalamu wa kufanya MATANGAZO YA KULIPIA basi, na akahakikisha anakua noma kiasi kwamba mtu akitaka kufanya matangazo ya kulipia anamcheki huyu mwamba.
So hivyo ndivyo ilivyo kuhusu NICHE na POSITIONING
NICHE ni KUNDI/SOKO ulilochagua, wakati POSITIONING ni namna/mtindo wa kuhudumia eneo dogo unalotaka kuspecialize kwenye niche husika.
Kwenye Maisha ya Kawaida Unaweza ukawa uko Vizuri sana na Familia Yako (mke/mme na watoto)
Tufanye mmekaa pamoja labda kwa miaka MITANO, kutokana na muda wote huo ukaanza kuhisi kumchoka mwenzako, au kumuzoea sana mpaka ukaona kama vile hakuna jipya. Ukaamua kuongeza MCHEPUKO mmoja.
Kitendo hicho unaweza kuhisi kitakuongezea FURAHA, lakini kiuhalisia kitakuongezea WASIWASI, utaanza kubadili mfumo wa maisha na kuanza kuwa msiri.
TUACHANE NA MAHUSIANO tuongee kwenye BIASHARA,
Kuna Muda Biashara/Huduma yako Moja au Ya Kwanza inakua kwa kasi na kuanza kuingiza pesa nyingi sana, watu wanaanza kuongezeka kwenye Circle yako, wengine wanataka partnership wengine wanaanza kukushirikisha Fursa zingine, MARA GHAFLA unaanza kuhisi hicho kinachotokea ni Mazingira ya Kupata Pesa Nyingine.
Mtu wa Mungu hicho kinachokutokea kwa asilimia zaidi ya 70% ni Mazingira ya kupoteza pesa,
Ukitaka kuelewa Vizuri, kumbuka namna ulivyoanza na ulivyokuza Biashara Yako ya Mwanzo, kulikua na Mazingira gani? Kuna mtu alihitaji kupartner na wewe? Kuna mtu alikushirikisha Fursa? Utagundua kwamba hakukua na hizo nafasi zote wala mambo hayo.. sasa kwanini yake sasahivi? (Akili kumkichwa)
Badala ya kutengeneza Pesa Utapoteza pesa.
SWALI NI JE UMETENGENEZA MAZINGIRA YA KUPATA PESA? Kwa maana kuwa na pesa nyingi hakumaanishi kwamba unaweza kuanzisha biashara yoyote na ikafanikiwa.
MAZINGIRA gani umetengeneza?
Nitakuambia Siku Nyingine Mazingira ya Kutengeneza Pesa, siku nikifanikiwa kutengeneza hizo pesa, kwasasa nafahamu mazingira ya kupoteza Pesa sababu Nimeishapoteza sana..
.
HIVI HAPA NI VIASHIRIA VYA MAZINGIRA YA KUPOTEZA PESA
1: Endapo Mazingira yakiwa tofauti kabisa na Mazingira ya mwanzo ambayo yalikupa pesa kwa zaidi ya asilimia 50% ujue hayo ni mazingira ya kupoteza pesa.
2: Endapo ukiona Hakuna Uhusiano Wowote kati ya NJIA za kufanikiwa kwenye huo Mchongo Mpya na Ule Mchongo wako wa Mwanzo ambao umefanikiwa tayari, basi ujue huu Mchongo mpya una UWEZEKANO mkubwa wa kukupotezea PESA..
Nina Experience ya Hii Kitu, nishapoteza sana. (Haha haha)
Most People Watasema Instagram, nafahamu ni kwasababu Wengi Wameishajaribu au huwa wanafanya matangazo Instagram HAWAJAWAHI kujaribu kufanya Matangazo YouTube 😎
Kitu usichojua ni kwamba, Tangu 2022 Youtube wamekua wakitransform kutoka kwenye Video Sharing & Searching Platform to Social Media platforms na hivi karibuni wanaelekea kwenye Peak..
Unajua Instagram & Youtube zimekua built-in by different Algorithms, yaani iko hivi..
Ukiweka Video on Instagram ndani ya masaa matano Engagement huwa inakua kubwa baada ya masaa matano huwa inaanza kushuka na baada ya masaa 24 unaweza usipate engagement tena kwenye Video hiyo.
Ukiweka Video hiyo Youtube, Engagement huwa inaanza taratibu na inazidi kupanda kadri watu wanavyoengage, na inazidi kwenda Viral kadri watu wnaavyointeract nayo hata kama ni zaidi ya Mwaka
Searching Option ya Instagram haipo Accurate based on Keywords na haina option ya Kufilter kwamba nataka Contents tu, video tu, post tu, reels tu, Account tu etc.. LAKINI searching option ya YouTube ipo more accurate based on Keywords na ina option ya Kufilter..
Actually najua haya huwezi kuyaelewa.. labda hiki hapo mbele unaweza kukielewa kirahisi..
Watanzania wameanza kufanya matangazo kwenye Instagram around miaka ya 2018, sasahivi karibia kila Mfanyabiashara anajua kufanya matangazo Instagram, na kufikia 2028 Wafanyabiashara asilimia zaidi ya 70% watakua wanafanya matangazo Instagram
Wafanyabiashara wa Tanzania wanaofanya matangazo YouTube ni kama asilimia 5% tu, ndio maana hukutani na matangazo ya wabongo huko.
Hapa napo unataka nikuambie hii ina maanisha nini??
Unajua ile Feeling ya kuwa Wakwanza kwenye Jambo fulani..? Usikaze ubongo aliyewahi amewahi.
Ukianza kuichukulia serious Youtube kuanzia sasahivi muda ambao usindani wa kibiashara huko sio mkubwa, na kipindi hiki engagement yake inaongezeka hasa kupitia kipengele chao cha Shorts.
I am sure watu wakija kushituka wewe utakua mbali sana.
Makundi ya Biashara hizi: Watoa huduma za afya (hasa wale wa Nguvu za kiume na mambo ya uzazi) au wauza bidhaa za afya, wauza bidhaa za urembo, watu wa kutoa consultation katika maswala ya uchumi na biashara.. na makundi mengi yanayofanana na hayo.. Youtube is your Thing, Take it serious..
Unahitaji tu kuwa na Simple Website From Google site, Au Kwa na Google Profile au Kutumia hizi Landing Pages mfano ya Leadspages, Wix, Stysteme.io nk
And Good news ni kwamba sio Lazima uwe na Laptop ndio ufanye Ads on Youtube, unaweza kufanya kwa kutumia SIMU YAKO..
Watu wa bidhaa za kawaida kama Vyombo, Nguo nk, niko naendelea kutafuta namna mnavyoweza kuitumia YouTube kuattract wateja wenu directly to WhatsApp
Nitakuja kuwaambia hapa nikipata Namna 😎
Mpaka Sasa Ili Kupata Good Results katika Platform ya Youtube Ni Lazima Uwe Na kitu Kimojawapo kati ya Hivi,
Simple Website From Google Site | Google Shop | Google Business Profile | Address on Google Map
Ukiwa na kimojawapo kati ya hivyo Vinne kulingana na biashara/huduma yako, Ukifanya Matangazo YouTube Utapata Big&Crazy results.. 🔥🔥🔥
SALES FUNNEL/LANDING PAGE inaweza kukusaidia kwa asilimia kubwa kupata matokeo mazuri LAKINI pia inaweza kupelekea wewe KUCHOMA PESA zako nyingi kwenye matangazo bila kupata matokeo
UnapoSet Matangazo kwenye Meta Ads Manager ukiweka LANDING PAGE au SALES FUNNEL yako kama Destination basi hakikisha setting zifuatazo uneziset Proper kabisa..
1: META PIXEL, hakikisha umeset DATASET vizuri, baada ya kuset Pixel kwenye site yako, Njoo kwenye Event Manager Set Event Vizuri kwenye Dataset yako.
2: UTM PARAMETERS, ukimaliza kuset Events zako ambazo unataka ziwe tracked, hakikisha unaset Parameters zako vizuri..
3: TUMIA GOOGLE ANALYTICS, ni muhimu kuconnect site yako kwenye Google anaytics, set vizuri kabisa Google Tag ili iwe rahisi kufahamu na Kutrack Visitors kwenye SITE yako.
KWANINI NI MUHIMU KUSET MAMBO HAYA?
iko hivi, usikaze ubongo sana, kama utategemea pekee data unazosoma kwenye Meta Ads Manager huwezi kuwa na uhakika kwamba WEBSITE yako inaconvert wateja.
Unaweza jikuta unatumia SALES FUNNEL lakini bado hupati wateja kabisa,
LAKINI ukiset vitu hivyo, itakusaidia kufahamu changamoto hasa ipo wapi,
Je ipo kwenye Tangazo ulilotumia,?
Je ipo kwenye Setting ulizoset?
Je ipo kwenye Landing page au sales Funnel yako?
Hizo data zitakupa majibu ya uhakika na utajua unatakiwa kufanya nini..
Mfano:
tangazo limekupa Link Clicks 5000+
Event inasoma 3000+ page views
Lakini hujui watu wangapi wamefika sehemu ya mwisho kwenye Landing Page/sales funnel yako
Hujui Watu wangapi wamevisit site yako
Hujui watu wangapi wamebonyeza BUTTON zilizo kwenye site yako..
Sasa kama hujui kuset mambo hayo, au unataka kufanya evaluation ya Landing page au sales Funnel yako nicheki nikusaidie.. (NOT FREE)
Kuna muda inaweza kuwa ngumu sana kumpa mtu matokeo mazuri na ya uhakika kwenye mitandao ya kijamii bila kutumia LANDING PAGE au SALES FUNNEL
Kwani LANDING PAGE ni nini?
Iko hivi, landing page ni ukurasa maalumu (Web-Page) ambao unakua na Taarifa muhimu pekee ambazo zinaaminika kumsaidia Mteja anayefikia kwenye ukurasa huo kuweza Kumfahamu Vizuri Muuzaji, kumuamini pamoja na kuelewa vizuri huduma atakayopatiwa
Wakati katika SALES FUNNEL ni web-page ambayo inakua katika STAGES Maalumu ambazo zinampitisha Mteja katika kumsaidia kufanya Maamuzi ya Kununua Au kulipia bidhaa au huduma
Kwahiyo wewe kama Social Media Manager ni muhimu sana kujua jinsi ya kutengeneza na kutumia hivi vitu kwasababu kuna baadhi ya Biashara ni Lazima kutumia Landing Page au Funnel ili kupata matokeo
Hasa ukikutana na Biashara za Level ya KATI au LEVEL YA JUU hizi ni muhimu sana kutumia Landing Page..
Kama mpaka muda huu hujui kutengeneza Landing Page au SALES FUNNEL book appointment na mimi... (NOT FREE)
2025 @ akilikubwa